May 5, 2020


HARUNA Niyonzima, kiungo anayekipiga ndani ya Yanga amemtaja mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere kuwa ndiye mchezaji wake bora zaidi wa kigeni ambaye amewahi kucheza Ligi Kuu Bara.

Niyonzima na Kagere wote ni raia wa Rwanda, waliwahi kucheza pamoja ndani ya Simba katika msimu wa 2018/19 na kufanikiwa kuipa timu hiyo ubingwa wa Ligi Kuu Bara pamoja na Ngao ya Jamii.

Pia katika msimu huo, Simba ilifika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Niyonzima katika kumtaja mchezaji wake bora wa kigeni kuwahi kucheza Ligi Kuu Bara, alisema: “Kwa upande wangu mchezaji bora zaidi wa kigeni ambaye amewahi kucheza Tanzania ni Meddie Kagere na hii ni kwa sababu hajakaa sana Tanzania ila amethibitisha ubora wake bila kuyumbishwa na watu.

“Nakumbuka tangu yuko Rwanda watu walikuwa wakimwita babu, lakini hajawahi kuyumbishwa na hilo bali amekuwa akifanya kazi yake uwanjani.

“Nadhani kila mtu anaona jinsi ambavyo amekuwa kwenye kiwango bora kwa muda mrefu na kitu nilichokipenda mimi ni kwamba hakuchelewa kuzoea mazingira ya Tanzania,". amesema.

Kagere ambaye msimu uliopita aliibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara baada ya kutupia kimiani mabao 23, msimu huu mpaka ligi inasimamishwa Machi 17, alikuwa amefunga mabao 19.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic