May 5, 2020


UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa hauna mpango wa kurejea kambini kwa sasa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vimesababisha ligi kusimamishwa ili kupisha maambukizi hayo.

Ligi ilisimamishwa Machi 17 kupitia kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mei 3, Rais Magufuli alisema kuwa anafikiria kurejesha ligi pale hali itakapokuwa shwari.

Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa licha ya kauli ya Magufuli hawana  mpango wa kurejea kambini.

"Tumeipokea kauli ya Rais kwa furaha lakini hatuna mpango wa kurejea kambini kwa kuwa hali bado haijawa shwari hivyo ni maombi yetu mambo yawe sawa ndipo tutarejea kambini.

"Bado vijana wapo nyumbani wanafanya mazoezi yao ili kuendelea kujiweka sawa kwani mazoezi ni muhimu kuendelea kwa kila mmoja kwa wakati huu," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic