May 22, 2020


PARIS Saint-Germain (PSG) inaripotiwa kuwa imeanza hesabu za kuwania saini ya mshambuliaji wa Arsenal, Pierre Emerick Aubameyang.

Aubameyang amekuwa kwenye ubora wake baada ya kujiunga na washika bunduki hao mwaka 2018 akitupia mabao 61 kwenye mechi 97.

Mshambuliaji huyo hajakubali kusaini dili jipya ndani ya Arsenal inayotumia Uwanja wa Emirates anaweza kusepa hapo mwishoni mwa msimu licha ya kuwa mkataba wake umebakiza mwaka mmoja.

PSG inaamini itapata saini ya nyota huyo mwenye miaka 30 kwa ada ya pauni milioni 45 kwa mujibu wa le10sport.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic