OFISA Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara, ameushauri uongozi wa Klabu ya Yanga kujiandaa vizuri kama ni kweli wanataka kuingia katika mabadiliko ya mfumo wa kiuendeshaji wa klabu yao.
Hivi karibuni, Yanga walikuja na kampeni iliyopewa jina ‘Twenzetu Kwenye Mabadiliko’ wakiwa na dhamira ya kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo unaosimamiwa na mdhamini wao, Kampuni ya GSM.
Akizungumzia hatua hiyo, Manara alisema: “Kwanza napenda kuwapongeza kwa hatua ambayo wanataka kuiendea.
“Lakini pia napenda kuwakaribisha huku tulipo kwa kuwa Simba tayari ilishapita hatua hiyo na yote kwa yote napenda kuwaasa watani zangu Yanga wajiandae vya kutosha kwani mchakato huu siyo rahisi na unahitaji weledi wa kutosha ikiwemo kubadilisha mtazamo wa kifikra.








Acha mdomo manara,zungumzia Simba tu,ni vyema ukatuacha na Yanga yetu coz Simba hamna cha kuishauri Yanga wakati nyinyi wenyewe mpaka sasa hakuna mabadiliko yeyote mliyofanya ya kiuendeshaji,Simba bado mpo kwenye mfumo uleule wa zamani wa kumtegemea mzamini,hadi sasa Simba inamtegemea mo km mfazili na si muekezaji..wakati wowote anaweza akawatupa na mkarudi kuombaomba km mwanzo..Hivyo manara kaa kimyaa,usipende kuropoka ropoka..ndio mana umekimbiwa na mke kwa mdomo wako..kudadadeki.
ReplyDeleteManara hana akili kwani simba imebadilika nn wakati inaendeshwa kwa mfumo wa ufadhili.Aachane na yanga azungumzie timu yake
ReplyDeleteNyie mikia hamuelewi rudun shule.ni sawa na manyumbu tu
ReplyDelete