May 10, 2020


UONGOZI wa Simba umesema kuwa iwapo Klabu ya TP Mazembe inahitaji huduma ya kiungo wao fundi Jonas Mkude wafike mezani wajadili biashara.

Imekuwa ikielezwa kuwa Mkude ameingia kwenye rada za timu hiyo ya Mazembe inayoshiriki Ligi Kuu nchini Congo ambayo imevutiwa na uwezo wa nyota huyo mzawa.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kutajwa kwa nyota wao kuhitajika na timu za watu wa Congo ni dalili kwamba kuna wachezaji wazuri ndani ya Simba.

"Hivi sasa dunia imebadilika hakuna tena mambo ya kuwazuia wachezaji kuhama ndani ya klabu hivyo ikiwa TP Mazembe wanaotajwa kuwania saini ya Mkude Kamati ya Wakurugenzi imesema waje mezani, ili ofa iskilizwe" amesema.

Mkude amefunga mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao kati ya mabao 63 yaliyofungwa na Simba ambayo inaongoza ligi ikiwa na pointi 71.  

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic