UONGOZI wa Yanga umesema kuwa mashabiki wanapaswa waendelee kujipatia nakala ya jarida la timu yao ili kujifunza mengi zaidi.
Hivi karibuni Yanga ilizindua jarida lao maalumu ambalo lina malengo ya kuwapa habari wanachama wao pamoja na mashabiki.
Ofisa Uhamasishaji na Msemaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa ndani ya jarida hilo kuna mambo mengi ambayo yatakuwa ni faida kwa wanachama pamoja na wapenzi wa klabu hiyo.
"Ni jarida zuri na maalumu kwa ajili ya wanaohitaji kupata taarifa zaidi za Yanga pia ni muhimu kujivunia kilicho bora, bei yake ni sh 5,000 ila ukinunua na jezi yenye chapa ya GSM ile orijino unapewa na jarida bure," amesema.







Watu hawana pesa ya kula. Mtu anataka watu wanunue kijarida 5000,?Aliyeshiba hamjui mwenye njaa. Hali ngumu kwa sababu ya Corona. Watu wanakosa pesa,ajira zinasumbua halafu wajinga fulani wanataka tununue kijarida.Bad timing. Tumieni akili.
ReplyDeleteNi ubunifu mzuri katika kuiingizia klabu mapato.Kuna hitilafu moja nimeiona kwenye ile app mpya ya klabu.Kata ya Ubung haipo kwenye orodha iliyowekwa.Watu wa ubungo tunalazimika kujaza kata tusizoishi ili kupata access ya kujisajili.Naomba lifanyiwe kazi hili.
ReplyDeleteAhsante