June 22, 2020


UONGOZI wa Azam FC, umesema kuwa kinachowaponza Azam FC kushindwa kufikia mafanikio ya kusepa na pointi nyingi uwanjani ni maamuzi ndani ya uwanja.

Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria amesema kuwa ndani ya msimu mmoja wameyeyusha zaidi ya pointi 15 kutokana na kutokuwa na maamuzi sahihi ndani ya uwanja.

Jana, Juni 21, Azam FC ililazimisha sare ya bila kufungana bao na Yanga ndani ya dakika 90 jambo ambalo limewafanya Azam FC wakusanye pointi 58 ikiwa imecheza mechi 30.

"Tumekuwa kwenye mazingira magumu ndani ya msimu huu, kuna pointi 15 ambazo tumepoteza kutokana na maamuzi yasiyo pendeza, nina amini kwamba ni lazima kuwe na usawa katika hili ili kupunguza masuala ya malalamiko.

"Ushindi ndani ya uwanja ni bao moja tu, nina amini mchezo wetu dhidi ya Yanga tulishinda ila mwisho wa siku maamuzi ndo yameamua tupoteze pointi mbili.

"Kuna mchezo ambao tulicheza na Tanzania Prisons ila mwisho wa siku tulifungwa bao tata usiku kutokana na maamuzi yaliyofuata haki na tulikubali kugawana pointi mojamoja na Prisons," amesema.

3 COMMENTS:

  1. Kwa maamuzi ya jana ni kweli mlishibda ila marefa waliamua kuibeba yanga, sijui ni kukosa kwao umakini au masuala ya miamala!!!!

    ReplyDelete
  2. Makanjanja kimyaa. Ingekuwa ni Simba suala hilo lingepelekwa hadi bungeni.

    ReplyDelete
  3. Hata waandishi wao waliokuwa wanaikomalia simba wamekaa kimya kabisa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic