June 22, 2020



MKURUGENZI wa masuala ya Ufundi ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) Oscar Milambo amesema kuwa ni mpango mkubwa uliopo kwa sasa ni kuendeleza vipaji kwa vijana ili waweze kufikia malengo ambayo wamejiwekea.

Milambo amesema kuwa ili kuwa na timu bora kwa taifa ni lazima kuwekeza kwa vijana jambo litakalosaidia kuwa na chaguo la wachezaji wengi.

"Muhimu kuwa na vituo vingi nchini ambavyo vitasaidia kukuza uwezo wao na kuendelea kuwalinda wakati wanaendelea kukua.

"Malengo yetu kwa sasa ni kuona kwamba kwenye kila mkoa kuna kuwa na shule maalum ambazo zitasaidia kuendeleza vipaji vyao na itasaidia kuwa na hazina kubwa kwenye timu ya taifa," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic