AZAM FC, Julai Mosi, Uwanja wa Taifa itakuwa na kazi ya kumenyana na Simba kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho.
Mchezo huo awali ulitarajiwa kuchezwa majira ya saa 10:00 Uwanja wa Taifa ila ratiba ya muda imebadilishwa.
Taarifa iliyotolewa leo imeeleza kuwa muda wa mechi hiyo utakuwa ni saa 1:00 usiku ila tarehe itabaki kuwa ileile ya Julai Mosi.
Azam FC inashuka uwanjani akiwa ni bingwa mtetezi wa taji hilo.
Mshindi wa mchezo huo atamenyana na mshindi wa mchezo kati ya Yanga na Kagera Sugar hatua ya nusu fainali.
0 COMMENTS:
Post a Comment