June 29, 2020


MAPINDUZI Balama amesema kuwa anajiskia faraja kuona wachezaji wenzake na mashabiki wanamuombea apone.

Mapinduzi aliumia kifunda cha mguu kwenye mazoezi walipokuwa wanajiandaa na mchezo dhidi ya Ndanda FC uliochezwa Uwanja wa Taifa.


Kwenye mchezo huo, Yanga ilishinda mabao 3-2 na kuwafanya wasepe na pointi tatu kibindoni na kujikusanyia jumla ya pointi 60 wakiwa nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 32.

Balama amesema:"Ninashukuru kuona wachezaji wenzangu pamoja na mashabiki wananiombea dua ili nipone, nina amini kwamba nitarejea kwenye ubora."

Balama ametupia mabao matatu ndani ya msimu huu wa 2019/20 na ana pasi moja ya bao kati ya mabao 38 yaliyofungwa na Yanga.

1 COMMENTS:

  1. Choma sindano ili ukaipambanie yanga shirikisho kama mlivyomfanya morison kwenye game ya simba,Morison pancha tupu yule ndiomana akicheza game moja atakaa benchi game tatu sasa huo si uhanisi jazbend,yanga nyinyi ni wauaji tena hamfai hata kulumangia.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic