MADA Maugo,bondia wa ngumi za kulipwa amesema kuwa haijui ladha ya chai na maandazi kwa muda wa miaka 12 sasa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Maugo amesema kuwa aliacha kunywa chai mwaka 2008 kutokana na ushauri aliopewa na daktari.
“Niliacha kunywa chai na maandazi tangu mwaka 2008 baada ya kushauriwa na waatalamu wa afya kuwa hakuna faida kwangu kutokana na kazi ambayo ninaifanya ya kupanda ulingoni.
“Ninachokifanya kwa sasa ni kula vyakula vya asili ikiwa ni pamoja na mihogo ili kuona namna gani ninaweza kulinda afya yangu kwani kikubwa ni kuwa na afya bora muda wote,” amesema Maugo.
|
June 28, 2020
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 COMMENTS:
Post a Comment