June 23, 2020


MWENYEKITI wa Bodi ya Ligi Tanzania, Almas Kasongo amesema kuwa wamepokea barua ya malalamiko ya Klabu ya Azam FC iliyopelekwa kwenye dawati lao.

Juni, 21 Azam FC ilikaribishwa na Yanga, Uwanja wa Taifa kwnye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao ulikamilika kwa sare ya bila kufungana.

Kasongo amesema kuwa wamepokea barua kutoka uongozi wa Azam FC leo wataijadili pamoja na kujadili matukio mengine ambayo yametokea kwenye Ligi Kuu Bara na Ligi Daraja la Kwanza.

"Tumepokea barua kutoka Azam FC ambayo inaeleza kuhusu mechi yao ya iliyochezwa dhidi ya Yanga, Uwanja wa Taifa, leo kamati itakutana ili kujadili kwani kazi yetu ni kufanyia kazi matukio ambayo yanatokea na kutoa adhabu kwa mujibu wa kanuni," amesema.

Kwenye barua ambayo Azam FC imeandika kwenda Bodi ya Ligi imeeleza kuwa hawajaridhishwa na maamuzi ya waamuzi wa mchezo huo ambao walikuwa ni Heri Sasi, mwamuzi wa kati na wasaidizi wake wawili wa pembeni Soud Lila na Mbaraka Haule.

Imeeleza kuwa malalamiko hayo yanatokana na bao lililofungwa dakika ya kwanza na Abdalah Kheri na lile la pili lililofungwa na Never Tigere dakika ya 47 yalikataliwa kwa kuelezwa kuwa ni ya kuotea pamoja na penalti baada ya Nico Wadada kuangushwa eneo la penalti.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic