June 23, 2020


Timu ya Coastal Union iliyo chini ya Kocha Mkuu, Juma Mgunda imeshaanza kuyazoea mazingira ya Mwanza baada ya kutia timu rasmi tangu jana.

Leo, Juni 23 itashuka Uwanja wa Kirumba kusaka pointi tatu mbele ya Mbao FC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Fred Felix Minziro, Minziro maarufu kama Baba Isaya.

Mgunda, nyota wa zamani wa Wagosi wa Kaya, amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo na watapambana kusaka pointi tatu.

Mchezo wake uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ilikubali sare ya bila kufungana huku Mbao FC ikitoka kupokea kichapo cha mabao 2-0 mbele ya Azam FC.

Coastal Union iko katika Top Five ya Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 48 ambazo tayari zinaihakikishia kubaki Ligi Kuu Bara kwa ajili ya msimu ujao huku Mbao FC ambao ni wenyeji wakiwa katika wakati mgumu katika nafasi ya 19.

Mbao mkononi wana pointi 23 tu, wakiwa wameshinda mechi 5 tu katika mechi zote 30 walicheza. Wamepoteza 17 na kupata sare 8, hali inayoonyesha wazi hawako katika hali nzuri na wanapaswa kujitutumua kiume hasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic