June 23, 2020


MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa waliokuwa wanawabeza baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 mbele ya KMC wasitarajie watafungwa leo mbele ya Ndanda FC.

Ndanda inayonolewa na Kocha Mkuu, Meja Mstaafu, Abdul Mingange itashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kushinda bao 1-0 mbele ya Biashara United, Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Leo, Juni 23, Ruvu Shooting itakuwa na kazi ya kumenyana na Ndanda Uwanja wa Mabatini, majira ya saa 10:00 jioni huku tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona ikiendelea kuchukuliwa.

"Niwakumbushe kwamba ukiachana na sare tuliyopata mbele ya Simba, tulifungwa mabao 2-1 na KMC ila haina maana kwamba na leo tutafungwa na Ndanda hilo halipo, muhimu kujua kwamba tunaendelea kupapasa.

"Kocha Mkuu, Salum Mayanga amenihakikishia kwamba wapo vizuri na wachezaji wana morali kubwa hivyo hakuna cha kuhofia mashabiki wajitokeze kuona namna gani Barcelona ya Bongo inatoa burudani," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic