June 18, 2020




UNAPOITAJA Singida United, kwenye maskio ya wanamichezo kwa wakati huu picha kubwa ambayo inawajia ni kuporomoka ghafla kwa timu hiyo yenye maskani yake mkoani Singida.
Wanajivunia uwepo wa zao la alizeti ambalo kwao ni nembo yao ni mwendo wa mwana kulipata mwana kulitaka lazima aitambue nembo yao na balaa lao uwanjani.
Msimu wa 2017/18 ilikuja kwa kasi na kujiwekea ufalme wake kwa kwenye upande wa soka la miguu jambo ambalo wengi waliamini kwamba kuna mtawala mpya anakuja.
Ushindani mkubwa ambao walianza nao uliwafanya wengi waanze kufikiria kuishangilia timu hiyo huku wachezaji wakiongeza kichwani timu ya nne kuwa pendwa kwao ukiachana na Simba, Yanga pamoja na Azam FC.
Kuanzishwa
Ilianzishwa mwaka 1972 ambapo ilikuwa inaitwa Mto Sports Club mwasisi wake anatajwa kwa jina la Elisamweli Elisamweli (marehemu) . 1990 ilikuwa miongoni mwa timu zenye majina kwenye Ligi daraja la Kwanza.
Kupanda daraja
Ilishiriki kwa mara ya kwanza Ligi Kuu Bara msimu wa 2000 ila ilishuka msimu wa 2001.
Ikiwa chini ya Kocha Mkuu Felix Minziro Baba Isaya ilirejea tena ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18.
Mafanikio
 Kushiriki Kombe la Shirikisho msimu wa 2017 kwa kutinga hatua ya fainali ambapo ilicheza na Mtibwa Sugar. Ilipoteza kwa kufungwa 3-2.Ilitinga fainali kwa kuitungua Yanga kwa penalti 4-2 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 Uwanja wa Namfua.
2017/18 ilimaliza ligi ikiwa ndani ya 10 bora ambapo ilikuwa nafasi ya tano na kibindoni ilikuwa na pointi zake 44. Ilishinda mechi 11, sare mechi 11 huku ikichapwa mechi nane na ilifunga jumla ya mabao 30.
Msimu wa 2018/19 ilimaliza ligi ikiwa nafasi 13 baada ya kucheza mechi 38 ilishinda 11 kichapo mechi 14 sare 13 na pointi zake 46 pointi hizo ziliiokoa isishuke daraja kwani ilikuwa kwenye mwendo wa kusuasua.
Uwanja
Uwanja wao wa nyumbani unaitwa Namfua ambao kwa sasa umebadilishwa jina unaitwa Liwiti.
Makocha waliopita hapo
Hans Pluijm alianza kukinoa kikosi baada ya kupanda ligi msimu wa 2017/18 ambapo alianza nacho kwa mafanikio makubwa kabla ya kuibukia Azam FC msimu wa 2018/19. Hemed Morroco aliinoa timu hiyo mambo yalipokuwa magumu aliibuka mseribia Dragan Popadic na Dusan Momcilovic ambaye alikuwa kocha msaidizi hawa nao wote walipigwa chini kutokana na matokeo mabovu ya timu na ilielezwa kuwa walikuwa wanawapiga makofi wachezaji.
Kosi lao matata hili hapa
 Ally Mustapha, Michael Rusheshangoga, Shafik Batambuze, Malik Antiri, Kennedy Juma, Mudathir Yahya
,Deus Kaseke,Kenny Ally,Lubinda Mundia,Tafadzwa Kutinyu, Salum Chuku, Peter Manyika, David Kisu, Miraji Adam,Salum Kipaga, Nizar Khalifan, Kigi Makasi, Papy Kambale na Danny Usengimana.
Hawa wametusua kupitia  Singida United
Mudhathir Yahya anakipiga zake Azam FC, Kaseke yupo zake Yanga,Kennedy Juma anakipiga Simba, Peter Manyika aliibukia KCB ila kwa sasa anakipiga Polisi Tanzania, David Kisu yupo zake Gor Mahia.
Ipo hapa
Imecheza mechi 29 imeshinda mechi tatu imepokea kichapo mechi 20 na imelezimisha sare sita zinazoifanya iwe na pointi 15 kibindoni  nafasi ya 20 ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Ramadhan Nswanzurimo ambaye aliweka wazi kuwa nafasi hiyo imetokana na wachezaji wake kushindwa kutimiza majukumu uwanjani.
Wakongwe hawa wanadunda
Haruna Moshi ‘Boban’ na Athuman Idd Chuji ni miongoni mwa wakongwe ambao waliwahi kukipiga Simba na Yanga na sasa wanaipambania Singida United.
Malengo
Kwa mujibu wa Cales Katemana, Ofisa Habari wa Singida United ameliambia Championi Jumatano kuwa hesabu zao kubwa kwa sasa ni kuipambania timu ibaki ndani ya ligi na mbinu kubwa ni kushinda mechi zote zilizobaki kisha mengine yatafuata.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic