June 18, 2020


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amewaomba mashabiki wa masuala ya michezo kumsamehe beki wa Klabu hiyo, Lamine Moro kwa kitendo kisicho cha kiungwana alichokifanya mbele ya nahodha wa JKT Tanzania, Mwinyi Kazimoto.

Moro alionekana akimpiga teke Kazimoto kwenye mchezo uliochezwa jana, Juni 17 Uwanja wa Jamhuri majira ya saa 10:00 jioni ambapo Yanga ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1.

Eymael amesema:"Ni jambo baya kwa mchezaji kulifanya ila hakukusudia, nimeongea naye na yeye mwenyewe amekiri kuwa amefanya makosa, katika hali ya kawaida anahitaji msamaha kwani mpira wa miguu una kanuni zake na kile alichokifanya amejutia.

"Ombi langu pia wadau wa masuala ya michezo mumpe msamaha kijana ameomba msamaha nina amini hatarudia na wale wengine wenye tabia kama zake iwe somo wasifanye makosa yanaumiza," amesema.

Moro amesema kuwa haikuwa dhamira yake ila ilitokea ghafla katika hali ya mchezo hivyo anahitaji msamaha.

3 COMMENTS:

  1. LAMINE MORO UMEFANYA KITENDO CHA KIKATILI SANA DHIDI YA NDUGU YANGU KAZIMOTO. ULIKUWA TAYARI APALALAIZI? AVUNJIKE KIUNO, AFE YOTE KWAKO SAWA KISA NI NINI KAKUKOSEA? NASUBIRI TFF WATAKUCHUKULIA HATUA GANI. BINAFSI MIMI NINGEKUWA KIONGOZI WEWE HUNA SIFA TENA KUCHEZA MPIRA BONGO UNA CHUKI ZA KUUMIZA WENZAKO. KWENYE MPIRA WACHEZAJI WANACHEZEANA RAFU WAKIWA NA MPIRA LAKINI WEWE UMEDHAMIRIA KWENDA KUMUUMIZA KUTOKEA NYUMA KWA MAKUSUDI UNAMKANYAGA KIUNONI WHYYYY? SAMAHANI YAKO NI KIINI MACHO. MWISHO NIWAOMBE JKT TANZANIA MCHUKUENI KAZIMOTO APELEKWE MUHIMBILI AKAANGALIWE INAWEZEKANA SANA ANA MAUMIVU YA NDANI YA MISHIPA. LAMINE MORO UMETUSIKITISHA SANA. WEWE HUMPENDI LAKINI SISI NDUGU WA KAZIMOTO TUNAMPENDA. NI MTU MSTAARABU SANA KAZIMOTO. UMEMUONEA TU.

    ReplyDelete
  2. An Open Letter to Mr. Lamine Moro.
    Sir, what you did to JKT Tanzania player Kazimoto is the most unsportsmanship sin ever seen in recent times in Tanzania soccer. Honestly you better find a better preoccupation that will give you respect. How can you harbor in your heart such hatred and come out to purposely hurt your fellow player in the field? I am totally lost. TFF and if need be FIFA could be consulted to usher some light on incidences of the like. You are simply letting us down as your fans.

    ReplyDelete
  3. OMG that was not football

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic