June 7, 2020


NICOLAS Wadada, beki wa Azam FC ni mhimili ndani ya kikosi hicho kutokana na uwezo wake anaonyesha ndani ya uwanja kwa kuzuia, kufunga na kutengeneza mashambulizi.
Raia huyo wa Uganda anakipiga pia ndani ya timu ya Taifa ya Uganda amekuwa ni injini ndani ya klabu hiyo ambapo kwa sasa yupo zake Uganda alikoibukia huko baada ya ligi kusimamishwa Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona.
Amecheza mechi 23, ambazo ni sawa na dakika 2,070 kati ya mechi 28 ambazo Azam FC imecheza ambazo ni dakika 2,520.
Akiwa amehusika kwenye jumla ya mabao nane kati ya 37 ambapo ametoa pasi saba za mabao na kufunga bao moja  ana wastani wa kuwa na hatari ndani ya lango kila baada ya dakika 258 na timu yake ipo nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi 54.
Ni mechi 16 washambuliaji hawakumzidi ujanja kupenya ngome yake, mechi 7 alizidiwa ujanja na washambuliaji walimpa tabu kwa kumuokotesha mlinda mlango wake mabao nyuma ya nyavu balaa lake ndani ya uwanja:-
Mechi zake za ushindi
Mechi zake za ushindi hizi hapa:- Azam 1-0 KMC, Polisi Tanzania 0-1 Azam FC, Ndanda 0-2 Azam FC, Namungo 1-2 Azam FC, Yanga 0-1 Azam FC, Biashara United 1-2 Azam FC, Singida 1-2 Azam FC, Mwadui 0-1 Azam FC, Azam FC 2-0 Lipuli, KMC 1-3 Azam FC, JKT Tanzania 0-1 Azam FC, Azam 1-0 Alliance, Azam FC 2-1 Ruvu Shooting na Polisi 0-1 Azam FC, Alliance 0-5 Azam FC.
Mechi zake za sare
Amekomaa na kupata sare nne ilikuwa mbele ya JKT Tanzania 2-2 Azam FC, Azam FC 0-0 Kagera Sugar, Mtibwa Sugar 1-1 Azam FC, Tanzania Prisons 1-1 Azam FC.
Hizi hapa alilala na viatu mazima
Mechi nne alishuhudia mlinda mlango wake akiokota nyavuni mipira:-Simba 1-0 Azam FC, Ruvu Shooting 1-0 Azam FC, Namungo 1-0 Azam FC ,Azam FC 2-3 Simba.
 Pasi zake za mabao
Idd Naldo (dk ya 15) wakati Azam ikiimaliza KMC bao 1-0 Uwanja wa Uhuru.
Mudhathir Yahaya (dk ya 48) wakati Azam FC ikiichinja kwa bao 1-0 Polisi Tanzania, Uwanja wa Uhuru.
Donald Ngoma (61) na Frank Domayo (90+1) wakati Azam FC ikiiua Namungo FC mabao 2-1 Uwanja wa Azam Complex.
Idd Seleman, ‘Naldo’ alikutana na pasi yake wakati Azam FC ikiimaliza kwa mabao 2-1 JKT Tanzania (dk ya 88).
Shaban Chilunda (dk 52) mbele ya Alliance wakati Azam FC ikishinda mabao 5-0.
Shaban Chilunda (dk 38) mbele ya Lipuli wakati Azam FC ikishinda mabao 2-0.
Kiungo chake hatari
Guu la kulia limetoa pasi tano za mabao, guu la kushoto limetoa pasi moja ya bao na kufunga bao moja hivyyo limehusika kwenye mabao mawili  na kichwa kimetoa pasi moja ya bao.
Guu lake la kulia limekuwa na hatari zaidi ambapo akiwa ndani ya uwanja licha ya kuwa na uwezo wa kutumia guu la kushoto pamoja na kichwa chake chenye rasta.
Hawa wamemjulia Wadada
Chilunda  na Naldo inaonesha wameanza kuwa na pacha tamu ambapo wote wawili wamemaliza pasi mbili alizowatengenezea kwa kujaza kimiani.
Nyota hao wote wawili walitumia pasi zilizopigwa kwa guu la kulia kuwaokotesha nyavuni makipa.
Pasi yake ya mapema
Dakika ya 15 kwenye mchezo wa kwanza wa ligi wakati huo Azam FC ikiwa chini ya Ettiene Ndayiragije alifungulia pasi yake ya kwanza iliyokutana na Naldo.
Pasi yake ya usiku
Kwenye mchezo dhidi ya Namungo FC alitoa pasi ya usiku dakika ya 90+1 iliyokutana na Frank Domayo.
Bao lake
Aliwatungua Biashara United, Novemba 8 kwa pasi ya kinara wa mabao ndani ya Azam FC, Obrey Chirwa wakati Azam FC ikishinda mabao 2-1.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic