Mechi ya kirafiki kati ya Yanga na KMC Uwanja wa Uhuru dakika 90 zimekamilika kwa Yanga kukubali kichapo cha mabao 3-0.
Mabao ya KMC yalifungwa na Sadallah Lipangile dakika ya 31, bao la pili lilipachikwa na Charlse Ilanfya dakika ya 45 na bao la tatu lilifungwa na Hassan Kabunda dakika ya 65 kwa mpira wa adhabu.
Mashabiki wamejitokeza kwa wingi kushuhudia mpambano huu wenye burudani za kutosha.
Msivunjike moyo. Kombe la FA ni lenu na ubingwa msimu huu na ujao wenu
ReplyDeleteKwa maneno ndio hata tembo kwa maneno anaweza kupaa lakini uwezo ndio utaamua.
ReplyDeleteMpira ni burudani,wote wametoka kifungoni
ReplyDeleteMmhhh
ReplyDeleteHuu ni mwaka wetu. Kichapo cha mbwa koko tumekipata, Molinga na wenziwe wamezidi kilo kumi kumi na Kocha anafanya ukorofi baada ya kupelekewa tiketi ya milioni 40. Mungu atusitiri na zomeo la mitaani
ReplyDeleteHivi nyaga waliweka mziki wote au masihara?
ReplyDeleteHivi nyaga waliweka mziki wote au masihara?
ReplyDeleteMuziki ni wote.Tatizo vitambi.
ReplyDeleteAlibaki kuingia mkwasa tu hao ndio GONGOWAZI
ReplyDeleteTunataka tuchukuwe ubingwa mara 5 mfululizo na fa mara 5 mfululizo waende wakavuwe kambare jangwani hao ndio GONGOWAZI
ReplyDeleteMpira wa magazetini ndio tatizo lake.Timu yetu bado mbovu sana.
ReplyDeleteTatizo haya magazeti ya kibongo yanatupamba sana,...... mara hoo Yanga hii ni balaa tupu Afrika, Mara ohhh kila atakaekuja mbele ya Yanga ni kichapo tu, wakati mpira wenyewe hatuuwezi kabisa. Timu yetu bado ni mbovu na wachezaji ni wabovu - wengine hawana hata uwezo wa kukaa benchi la yanga wafukuzwe
ReplyDeletepoleni xana 🐥🐥🐥 fc.
ReplyDeleteMadhaifu mengi yamejionyesha niliyajua haya yatatokea baada ya kusikia benchi halijakamilika makocha watatu muhimu kuleta fitness ya wachezaji hawapo..vile vile niliposikia timu haijaingia kambini pia niliposikia wachezaji wameongezeka uzito niliposikia mkurugenzi wa mashindano wa Yanga Anaitwa Thabiti Kandoro (Simba Damu) na kutokuwepo kwa mkurugenzi wa ufundi niliposikia nahodha ni majeruhi nilijua kuna siku majibu yake ya kupoteza mechi yatakuja...kwakweli kama hii ndiyo Yanga wenyewe hii....kweli Twenzetu kwenye Mabadiliko kwani 65% ya wachezaji wa Yanga hawastahili kuivaa jezi ya njano na kijani ya klabu hai kongwe kabisa, mabadiliko yaguse Sekretariati na baadhi ya benchi la ufundi....Twenzetu Kwenye Mabadiliko
ReplyDeleteMara hii na kikosi cha kichapo!!!! Hawa KMC hawana adabu kabisa
ReplyDelete