“Siyo kwamba mimi sina uwezo wa kuwa mfungaji bora kwenye ligi hii, ila kinachonisumbua ni suala la kuwa nje kwa muda mrefu jambo ambalo wengi hawataki kulikubali na kunipa muda, nimecheza timu nyingi kubwa ila niliumia na hiyo ndiyo sababu ya kupungua uwezo.

“Kama ningepata nafasi ya kuchezea Yanga tena msimu ujao basi naamini ningeweza kupata utimamu mzuri na hakika Yanga wangefurahia.

“Kwa sasa acha niondoke ila najua watakuja kunikumbuka maana ninakoenda nitapata muda mzuri wa kujiweka fiti na kufunga,” alisema Molinga.Ameeleza kuwa ameshasaini mkataba wa awali wa miaka mitatu kujiunga na timu hiyo ya Morocco kwa kuwa mkataba wake na Yanga unaelekea ukingoni.

“Unajua mimi sikusafiri kipindi cha Corona kwa kuwa Yanga walitaka kuzungumza na mimi kuhusu mkataba wangu, lakini haikuwa hivyo.

“Mara kadhaa imewahi kujitokeza nikiwakumbusha viongozi kuhusu mkataba wangu lakini nikawa nazungushwa tu, hivyo sikujua hatima yangu, mwisho nikachoka, nikaamua kusaini hiyo timu ya Morocco mkataba wa awali ambapo rasmi nitajiunga nao baada ya msimu huu."