June 20, 2020


UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa hawana hofu na Coastal Union licha ya kuwa ipo kwenye uwanja wao wa Mkwakwani, Tanga.

Mtibwa Sugar iliyo chini ya Kocha Mkuu Zuber Katwila, ipo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 33 baada ya kucheza mechi 29 itamenyana na Coastal Union majira ya saa 10:00 jioni.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema:"“Tunajua kwamba mchezo wao uliopita walipata sare ya kufungana mabao 2-2 mbele ya Namungo hiyo haitupi tabu kwani kikosi chetu kipo imara na kamili kuwavaa wapinzani wetu.

"Mbinu ambazo Katwila amewapa vijana zinatosha kutupa ushindi kilichobaki ni dakika tisini kuamua namna gani tunashinda, mashabiki wetu wasiwe na mashaka tunafanya kazi bila hofu," amesema. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic