HASSAN Kabunda, winga wa KMC amesema kuwa wamekubaliana kwa
pamoja kupambana ili wasishuke daraja msimu ujao.
Akizungumza na SpotiXtra, Kabunda alisema kuwa wapo kwenye
nafasi mbaya kwenye msimamo wa ligi jambo ambalo linawafanya wapambane kwa kasi
kurejea kwenye ubora wao.
“Tulianza kuwa bora kabla ya ligi kusimama kutokana na Virusi vya
Corona, lakini tumekubaliana kuendelea kupambana ili tusipate matokeo mabaya
yatakayofanya tushuke daraja msimu ujao, inawezekana kubaki na hatutaki kushuka
daraja,” alisema.
KMC ipo nafasi ya 15 kwenye msimamo imecheza mechi 29 na
imejikusanyia pointi 33 kibindoni, Juni 20 itamenyana na Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru.
0 COMMENTS:
Post a Comment