June 23, 2020


UONGOZI wa Simba umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho utakaochezwa Uwanja wa Sokone majira ya saa 10:00 jioni.

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja Mkuu wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa na wachezaji wapo tayari kwa ushindani.

"Wachezaji wanajua majukumu yao hakuna ambaye anafikiria kushindwa hivyo kazi kubwa kesho ni kusaka pointi tatu ndani ya uwanja, mashabiki wajitokeze kuona burudani," amesema.

Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 75 baada ya kucheza mechi 30.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic