INJINIA Hersi Said, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, amesema kuwa watarejea kimataifa kwa kupitia Kombe la Shirikisho ambalo lipo mikononi mwa Simba.
Katika Kombe la Shirikisho, Yanga imetinga hatua ya nusu fainali ambapo inatarajia kucheza na Biashara United ikiwa watashinda hapo wanaweza kukutana na mshindi wa mchezo kati ya Azam FC v Simba.
Injinia amesema:”Tutashiriki mashindano ya kimataifa bila kutegemea nafasi ya upendeleo na tutashiriki kupitia Kombe la Shirikisho, kumbuka kwamba tupo hatua ya nusu fainali na tuna amini kwamba tutashinda.
“Ikiwa tutachukua Kombe la Shirikisho basi hiyo itakuwa njia yetu kushiriki mashindano ya kimataifa. Kikubwa ni mashabiki kuendelea kutupa sapoti,” amesema.
Kwa upande wa Biashara United, kupitia kwa Ofisa Habari Idrisa Sechombo amesema kuwa kikosi chao kipo vizuri na wanaamini watapambana.
Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, Biashara United ipo nafasi ya nne huku wapinzani wao Yanga wakiwa nafasi ya pili.
The time will tell,ningekushauri upunguze kujiamin na kujigamba kiasi hicho,ina maana biashara,azam,simba,dodoma wao hawalitaki kombe hilo?unazidi kumtia hasira mnyama ili aje kukung'atia meno,nakuonea huruma sana mpendwa ila subiri siku yako inakuja utaimba nyimbo zote za utoto kipindi unacheza kombolela.
ReplyDeleteKwanini unasema hivi?
DeleteKufeli na kuteseka kwa Yanga ni huu wivu wa kutokubali kuwa Simba wapo level ya juu zaidi zidi katika kila idara hata wanakwenda mazoezi yao Simba wanaonekana wapo professional zaidi lakini Yanga wanatumia nguvu kubwa katika kubeza badala ya kujifunza. Wakijifananisha na timu ambayo kiukweli imeshapita level yao. Simba wamepambana kimataifa na jitihada za namungo na kupatikana nafasi nyingi kushiriki kimataifa msimu ujao basi bila ya kigugumizi ni kuwapa pongezi tu badala ya ujinga wa kukataa uhalisia.
DeletePointi yako imenivutia sana Ndg. Keya Said. Hakika umeongea kwa mantiki kubwa sana. Sambamba na wewe, mimi pia najiuliza kwa mshamgao kwamba mtu msomi wa kiwango cha Hersi Said anawezaje kushindwa kutambua kwamba kwa hadhi Kombe la CAF Shirikisho ( CAF Confederation Cup) lipo chini sana ya CAF Champions League. Hivyo, kwa timu kubwa yoyote barani Afrika, nguvu zote na juhudi zote huelekezwa kwenye kupata nafasi kucheza Champions league na sio Confederation. Ina maana kwamba Yanga akiwa mshindi wa pili wa ligi kuu ya VPL automatically ataungana na Simba kwenda Champions League. Huu ni ukweli usiopingika. Itakuwa ni maajabu, endapo Yanga atakuwa mshindi wa pili na pia mshindi wa TFF-AZAM Cup, halafu badala ya kwenda ligi ya mabingwa Afrika yeye akaamua kwenda ligi ndogo ya CAF Confederation Cup kama anavyosema huyu bwana Hersi Said. Ikitokea hivyo kweli tutaamini kwamba akili za Utopolo hazinagana tofauti ya aliyesoma na asiyesoma kama alivyowahi kusema Haji Manara wakati fulani. Yaani eti kwa ajili ya ushabiki maandazi wa kindezi ndezi hivi unakataa nafasi ya kushiriki mashindano ya juu Afrika kwa hofu kwamba utachekwa na mpinzani wako kuhusu mbeleko uliyobebwa. Kwanini usishiriki kwa hasira hadi kupata mafanikio makubwa ambayo utayatumia vizuri sana kumbeza mpinzani wako? Huoni kwamba kwa kuamua kushiriki mashindano madogo eti kwasababu hutaki kupoteza hadhi yako kwa mpinzani ndio kwanza unazidi kuwa na hadhi ndogo zaidi kwake? Sasa naanza kuamini kuamini kwamba kwa aina hii ya viongozi, itawachukua muda sana Yanga kupata kasi ya mafanikio kama wanayoenda nayo Simba.
DeleteNa kombe hilo la shirikisho waliorembuka kulipata na kuliota usiku na mchana ndio wanahusisha kuwa ndio chanzo kilichowawezesha kuingia mashindano ya klabu bingwa Afruca msimu ujao na wala sio Simba iliyowanyanyua. Hawajui kkitu kinachoitwa ahsante
ReplyDeleteHao kitu shukuru hawakijuwi yaani kula ulale tu
ReplyDeleteWachezaji wa nje wameiuza Yanga..hawana kiwango cha kuridhisha..wazawa ni Bora kuliko wa nje...
ReplyDeleteWote hao akili moja
ReplyDeleteBora amekubali kuwa ubingwa sasa basi. Lakini jee wakishika nafasi ya pili kwenye ligi na wakapata ubingwa wa FA watachagua kucheza confederation cup?
ReplyDeleteHaku a ubingwa wataoupara baada ya ule wanaiuimba kola wakati pale Mntama alipochezesha kikosi cha pili
ReplyDeleteWanao ubingwa wa mapinduzi cup.
ReplyDeleteDaima mbele nyuma mwiko...
ReplyDeleteBreaking News: Ligi daraja la kwanza (FDL) Tanzania msimu ujao 2021/22 - Mechi No.3
ReplyDeleteKorosho Vs. Simba uwanja wa Sijaona - Mtwara