June 27, 2020


UONGOZI wa Simba umeishukuru Serikali kwa kuruhusu mashabiki kuingia kwenye mchezo wao wa kesh dhidi ya Tanzania Prisons utakaochewa Uwanja wa Sokoine.

Serikali ilipiga marufuku mashabiki kuingia kwenye mechi zote za Simba na Yanga ambazo zitachezwa nje ya Dar es Salaam kutokana na muongozo uliotolewa kukiukwa kwenye mechi zao za hivi karibuni.

Simba kwenye mchezo wake dhidi ya Mbeya City uliochezwa Juni 24, mashabiki walijitokeza wengi na hawakufuata muongozo uliotolewa ikiwa ni pamoja na kukaa umbali wa mita moja kwa lengo la kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

Kutokana na jambo hilo, Serikali iliamua kuifungia Simba kucheza bila mashabiki ila kwa maombi maalumu ya na viongozi wa timu kwa Serikali ambapo Mbeya City iliomba msamaha kwa makosa hayo hatimaye Serikali imetoa kibali na kwa masharti maalumu.

Ofisa Habari wa Simba Haji Manara amesema:"Tunaishukuru Serikali yetu sikivu kwa kuruhusu mashabiki kuingia uwanjani Kesho hapa Mbeya.

"Mategemeo yetu ni kuona masharti yaliyowekwa yanazingatiwa."

1 COMMENTS:

  1. Afadhali maana walisafiri kutoka mikoa mbalimbali kuangalia mechi hizo. La muhimu maelekezo yazingatiwe na wahusika

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic