June 29, 2020


WACHEZAJI wa Simba, benchi la ufundi pamoja na viongozi wamerejea leo Dar es Salaam wakitokea Mbeya walipokuwa na kazi ya kucheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara.

Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck imecheza mechi mbili za ligi, ilianza mbele ya Mbeya City ambapo ilishinda mabao 2-0 na ikamalizana na Tanzania Prisons ambapo ilitoshana nguvu kwa kutoka sare ya bila kufungana.

Sare hiyo imewathibitisha kuwa mabingwa mara ya tatu mfululizo kwa kuwa imefikisha jumla ya pointi 79 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote ndani ya ligi.

Sven amesema kuwa walistahili kutwaa ubingwa huo kwa kuwa wachezaji walikuwa na juhudi ndani ya uwanja katika kutafuta matokeo pamoja na ushirikiano waliokuwa wanapewa kutoka kwa mashabiki.

Simba inafikisha ubingwa wa 21 kibindoni huku wakiwa wamezidiwa na Yanga ambao wametwaa taji hilo mara 27.

Kwa sasa wanajipanga kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho unaotarajiwa kuchezwa Julai Mosi, Uwanja wa Taifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic