June 28, 2020


NAHODHA wa Simba, John Bocco amesema kuwa wachezaji wamekubaliana kubeba ubingwa kabla ya kumaliza mechi zao zilizobaki mkononi ili kupunguza presha ya mechi zilizobaki.
Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 78 imebakiwa na mechi saba ili kumaliza mechi zake za mzunguko wa pili kwa msimu wa 2019/20.
Kwenye ushindi wa mabao 2-0 waliopata mbele ya Mbeya City, Bocco alitupia mabao yote na kumfanya afikishe jumla ya mabao saba kwenye ligi msimu huu.
Bocco amesema:” Malengo yetu ni kuona tunatwaa ubingwa tukiwa na mechi nyingine mkononi baada ya wote kukubaliana kufanya kazi kwa kujituma ila haitawezekana iwapo hatotapewa sapoti.
“Kushinda mechi yetu mbele ya Mbeya City ni jambo nzuri tuna kazi nyingine ya kucheza na Tanzania Prisons nao pia wapo vizuri hivyo kuna kazi nyingine mbele yetu ya  kufanya.”
Ikiwa Simba itashinda mchezo wake wa leo, Juni 28 Uwanja wa Sokoine itatwaa ubingwa mara ya tatu mfululizo kwa kuwa itafikisha pointi 81 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote kwa sasa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic