SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba, amesema kuwa kikubwa ambacho kinawabeba wachezaji wake kufanya vizuri ndani ya uwanja ikiwa ni pamoja na kufunga mabao ni pamoja na kutumia akili katika kila wanachokifanya kwa kutegemeana.
Wachezaji wa Simba ndani ya uwanja wanaongozwa na nahodha, John Bocco akishirikiana na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ ambaye ni nahodha msaidizi.
Akizungumza na Saleh Jembe, Sven amesema kuwa imekuwa ni kawaida ya wachezaji wake wote kushirikiana katika mambo ambayo wanayofaya jambo ambalo linawafanya kila mmoja kutumia akili ya mwenzake.
“Ukimtazama Bocco akiwa ndani ya uwanja anafanya majukumu pia ya ulinzi licha ya kwamba ni mshambuliaji na muda mwingine mtazame Wawa anafanya kazi ya ushambuliaji, hiki ni kitu kinachowafanya wachezaji kuwa bora kwa kuwa wanashirikiana.
“Ninapenda kuwashukuru mashabiki kwa namna ambavyo wanatupa sapoti katika mechi zetu tunazocheza ni kitu kizuri nasi tutaendelea kupambana ili kutoa burudani,” amesema Sven.
Simba imetwaa ubingwa wa ligi kuu mara tatu mfululizo ambapo kwa msimu huu imefanikiwa kufanya hivyo ikiwa imebakiwa na mechi sita mkononi baada ya kufikisha pointi 79.
0 COMMENTS:
Post a Comment