June 29, 2020


KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amewapongeza Simba kwa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa mara ya tatu mfululizo.

Simba ilikamilisha hesabu za kuwa mabingwa wa ligi, jana kwa kulazimisha sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine.


Eymael raia wa Ubelgiji amesema anawapa pongezi Simba kwa kuweza kutwaa taji la ligi.

"Hongera kwa Simba kutwaa taji la ligi kwa msimu huu wa 2019/20.

Pia Ofisa Muhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa watani zao Simba wanapaswa kupewa hongera.

"Hongerini watani zetu kwa kutwaa ubingwa wa ligi kwa msimu wa 2019./20."

Kwa sasa Yanga wamewekeza nguvu kwenye kutwaa taji la Kombe la Shirikisho ambapo kesho watakutana na Kagera Sugar Uwanja wa Taifa hatua ya robo fainali.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic