UONGOZI wa Klabu ya Azam FC umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar inayonolewa na Zuber Katwila.
Mchezo huo wa ligi unatarajiwa kupigwa Julai 15 Uwanja wa Gairo, Morogoro unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na vita ya nafasi kupamba moto.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na tayari maandalizi yameanza kuelekea kwenye mchezo huo.
"Tumeanza maandalizi kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Mtibwa Sugar na ninaamini utakuwa mchezo mgumu na wenye ushindani ila tunahitaji pointi tatu muhimu," amesema.
Mchezo wao uliopita wa ligi Azam FC ilishinda bao 1-0 mbele ya Mwadui FC Uwanja wa Azam Complex.
Ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 65 baada ya kucheza mechi 34 inakutana na Mtibwa Sugar iliyo nafasi ya 14 na pointi 38 nayo imecheza mechi 34.
0 COMMENTS:
Post a Comment