July 12, 2020

UONGOZI wa Simba umegoma kuweka wazi hali ya beki wa kulia Shomari Kapombe kwa sasa kwa kuwa imewekeza akili zake kwenye mchezo wa leo wa hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga utakaopigwa Uwanja wa Taifa.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza kupigwa majira ya saa 11:00 jioni na utahudhuriwa na mashabiki elfu 30 tu kwa kuwa ni agizo la Serikali katika kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa hawawezi kuzungumza kuhusu mchezaji wao kwa kuwa mchezaji alishaongea hivyo hakuna jambo jingine atakalosema.

"Nadhani mchezaji aliongea hivi karibuni na taarifa zake ziliwekwa pia kwenye akaunti ya Jembe hivyo sioni cha kuzungumza kuhusu Kapombe kwa sasa na hali yake, hata kuhusu mchezo wetu dhidi ya Yanga wapo wahusika wenyewe watazungumza," amesema. 

Kapombe alipata majeruhi ya mguu Julai Mosi Uwanja wa Taifa wakati Simba ilipokuwa ikimenyana na Azam FC alikosa mechi mbili za ligi mbele ya Ndanda FC pamoja na ule dhidi ya Namungo FC.

Hivi karibuni Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck alisema kuwa Kapombe atakuwa nje mpaka msimu ujao kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya  mguu.

Kapombe kwenye mahojiano na waandishi wa Habari alisema kuwa yupo fiti kwani alipata maumivu kidogo tu hivyo mashabiki wasiwe na mashaka naye.

Huenda Kapombe akaukosa mchezo wa Yanga leo Uwanja wa Taifa kwa kuwa hajawa na mechi fitinesi ila maamuzi ya kuanza ama kuanza yapo mikononi mwa Sven.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic