BIASHARA United ya Mara leo imelazimisha sare ya bila kufungana na Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Karume.
Mchezo wa leo Julai 5, ulikuwa na mvuto na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili ambapo zilikuwa zinacheza kwa kushambuliana kwa zamu huku uwanja ukionekana kuwa tatizo kwa Yanga pamoja na umakini wa kumalizia nafasi walizokuwa wakizipata.
Kiungo Haruna Niyonzima alishindwa kumaliza dakika 90 baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Abdulaziz Makame.
Yanga inafikisha pointi 61 huku Biashara United ikiwa imejikusanyia jumla ya mechi 45 zote zimecheza mechi 33.
Mashabiki wengi walijitokeza uwanjani ili kushuhudia mchezo wa leo ambapo mpaka dakika tisini hakuna timu iliyoona lango la mpinzani.
Kwenye mchezo wa kwanza Yanga ilishinda bao 1-0 lililojazwa kimiani na Tariq Seif Uwanja wa Taifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment