BAKARI Mwamnyeto, nahodha wa Klabu ya Coastal Union iliyo chini ya Kocha Mkuu, Juma Mgunda amesema kuwa watazidi kupambana ili kufikia malengo waliyojiwekea.
Beki huyo kipenzi cha Mgunda amekuwa Kwenye ubora wake msimu huu ambapo amekuwa kiongozi kwenye timu hiyo ambayo inaleta ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara.
Licha ya kuyumba hivi karibuni baada ya ligi kuendelea kwa kupokea vichapo vitatu mfululizo bado imesimama imara na kubaki nafasi ya tano.
Ilichapwa bao moja na Mbao FC Uwanja wa Kirumba, ikanyooshwa 1-0 mbele ya Alliance FC kisha ikakutana na kichapo cha mabao 3-1 mbele ya Mbeya City pale Sikoine.
Kesho, Julai 15 ina kazi mbele ya Kagera Sugar Kaitaba iliyo chini ya Mecky Maxime aliyetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Yanga.
Ipo nafasi ya tano Kwenye msimamo ikiwa na pointi 51 kibindoni baada ya kucheza mechi 34. Safu ya ulinzi imeruhusu mabao 27.
"Bado tutazidi kupambana kwani wapinzani wetu nao wanahitaji ushindi nasi tunahitaji pia ushindi," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment