INAELEZWA kuwa nyota wa zamani wa Azam FC, Kipre Tchetche ambaye anakipiga kwa sasa soka la kulipwa nchini Malaysia yupo kwenye mazungumzo na mabosi hao ambao wanahitaji kuboresha kikosi chao.
Tchetche mwili jumba mwenye nguvu nyingi anatajwa pia kuingia kwenye rada za Simba ambao nao wanatajwa kuhitaji saini ya nyota huyo.
Azam FC msimu huu imepoteza kila taji lililokuwa mkononi mwao jambo ambalo limewafanya viongozi kupasua kichwa namna ya kurejea upya msimu ujao wa 2020/21.
Walianza kuyeyusha taji la Mapinduzi lililobebebwa na Mtibwa Sugar kisha wakafuatia kulisindikiza taji la Shirikisho ambapo waliishia hatua ya robo fainali.
Kwenye mbio za ubingwa wa ligi, Simba ilimaliza kazi mapema kwa kutwaa taji ikiwa na mechi sita mkononi hivyo kwa sasa Azam FC wanapambania nafasi ya pili na mshindani wake mkubwa ni Yanga huku Namungo FC akiwa ni mshindani asiyeonekana kama ana makali ila ana jambo lake.
Ofisa Habari wa Azam FC Zakaria Thabit amesema kuwa kuna mpango mkubwa wa kufanya maboresho ndani ya kikosi ila ni mpaka wakati wa usajili utakapofika.
Huyu hana jipya, tupa huko. Tafitene straiker kijana sio huyu babu
ReplyDelete