USHINDI wa mabao 2-0 walioupata Dodoma FC unawapa tiketi ya kupanda moja kwa moja ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Dodoma FC inaungana na Gwambina ambayo ipo kundi B ambayo tayari nayo imeshakata tiketi ya kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/19.
Dodoma FC imepanda baada ya kufikisha jumla ya pointi 51 baada ya kucheza mechi 21.
Imewapiku wapinzani wake wa karibu Ihefu ambao nao wana pointi 51 tofauti yao ni kwenye idadi ya mabao ya kufunga. Dodoma wamefunga jumla ya mabao 38 huku Ihefu wakiwa na mabao 33. Hivyo Ihefu imepata tiketi ya kucheza play off ili ipate tiketi ya kushiriki Ligi Kuu Bara.
Hongera Dodoma kupanda vpl
ReplyDeleteHongera zao
ReplyDelete