July 11, 2020


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa nahodha wao Papy Tshishimbi yupo fiti kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Simba utakaochezwa Uwanja wa Taifa, Julai 12.

Mchezo huo hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila timu kuhitaji matokeo mazuri.

Ofisa Uhamasishaji wa Klabu ya Simba,  Antonio Nugaz amesema kuwa kila kitu kuhusu mchezo wa kesho kipo sawa wanasubiri wakati ili watoe burudani kwa mashabiki pamoja na soka safi.

"Tupo sawa na tutatoa burudani safi kwa mashabiki na malengo yetu ni kupata ushindi, bila makandomakando hatufungwi sisi, tupo vizuri na mambo yatakuwa uwanjani.

"Wachezaji wote wapo sawa kuanzia Tshishimbi yupo vizuri hivyo ni jukumu la mwalimu mwenyewe kujua anaanza na nani ila kikosi na wachezaji wote kiujumla wapo tayari tukutane Taifa kuona namna itakavyokuwa," amesema. 

Mshindi wa mchezo wa kesho atacheza na Namungo hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho itakayochezwa Sumbawanga. 

Tshishimbi alikuwa nje ambapo alikosa mechi za hivi karibuni ikiwa ni pamoja na zile mbili walizocheza mkoani kati ya Biashara United ambapo iliisha kwa sare ya bila kufungana pamoja na ile ya Kagera Sugar ambapo Yanga ilishinda bao 1-0  kwa kuwa alikuwa unasumbuliwa na goti.

Leo alikuwa  miongoni mwa wachezaji waliokuwa wanafanya mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa kesho.

7 COMMENTS:

  1. Kabla hujapost soma kwanza upya,..Ofisa Uhamasishaji wa Klabu ya Simba, Antonio Nugaz amesema kuwa kila kitu kuhusu mchezo wa kesho kipo sawa wanasubiri wakati ili watoe burudani kwa mashabiki pamoja na soka safi.

    .

    ReplyDelete
  2. Mtieni sindano kama mlivyomfanya Morison kwenye game ya simba,hakuna wachezaji yanga msipofanya hivyo lazima mkalishwe na mnyama,ila muwe makini sana maana baadae madhara yake ni makubwa sana,mchezaji atakuja kukaa benchi mwaka mzima kumbe ujinga mliufanya wenyewe,Morison mlimchoma sindano nne ili acheze mechi dhidi ya simba,chanzo cha habari hii yeye mwenyewe kupitia blog hii,punguzeni unyama maana huo sio ubinadamu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tulia ww dawa ikuingie....acha woga hata ulaya mambo ya mchezaji kuchomwa cndano ili acheze yapo...

      Delete
  3. Habari ya wachezaji was Yanga waachiwe Yanga wenyewe, we endelea na ya kwenu Simba. We jadili kama mtachoma sindano Kapombe ili acheze leo kitatokea nini, achana na timu ya wenye nchi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Utajua muda utakapofika,akipenda chongo huita kengeza.jipange kupokea maumivu leo taifa muda si mrefu tangu sasa.

      Delete
  4. Natamani Yanga iwe na wachezaji wake wote muhimu kwenye mechi ya leo ili wasiwe na visingizio watakaponyooshwa na MNYAMA.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic