July 9, 2020



SHOMARI Kapombe beki wa kulia wa Simba atakosekana kwenye mchezo dhidi ya Yanga utakaochezwa Uwanja wa taifa, Julai 12.

Mchezo huo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote kusaka heshima na rekodi ndani ya Uwanja wa Taifa.

Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa hatamtumia Kapombe kwa kuwa anasumbuliwa na majeruhi ya mguu ambayo yatamuweka nje kwa muda mpaka msimu ujao.

Kwa sasa kikosi cha Simba kimerejea Dar ambapo kilikuwa na mechi mbili nyanda za juu kusini walianza na ile dhidi ya Ndanda FC kisha wakamalizana na Namungo FC Julai 8.

Kwenye mchezo dhidi ya Namungo baada ya dakika 90 kukamilika huku matokeo yakiwa sawa na yale waliyopata mbele ya Ndanda kwa kumaliza bila kufungana walikabidhiwa kombe lao.

Kapombe alikuwa kwenye ubora wake msimu huu ambapo ametoa jumla ya pasi nane kwenye mashindano yote.

Ana pasi sita kwenye Ligi Kuu Bara huku akihusika kwenye pasi mbili ndani ya Kombe la Shirikisho.

Sven amesema:"Hajawa imara kwa ajili ya mechi zilizobaki ninadhani atakosekana kwenye mechi zetu ambazo zimebaki."

Inaelezwa kuwa nafasi ya Kapombe itazibwa na Shamte ambaye ameanza kuaminiwa na Sven ndani ya kikosi cha kwanza.

Kapombe aliumia mguu kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho wakati Simba ikishinda mabao 2-0 mbele ya Azam FC Uwanja wa Taifa, Julai Mosi.

5 COMMENTS:

  1. Frank Domayo roho kwatu kusikia haya ya Kapombe kushindwa kuonesha umahiri na utaalamu wake kwenye kandanda kwa nafasi yake muhimu kwenye kikosi. Alitumwa na shetani wake huyo aliyemtuma ataendelea kumtuma kufanya mengine yatakayomgharimu sana maishani

    ReplyDelete
  2. MUNGU ambariki ngoma, kwa ujinga alionao na roho yakipepo anayoikubali imtumie

    ReplyDelete
  3. Huyo Domayo, alichokifanya Ni makusudi mazima, roho mbaya tu, tena siyo mara ya Kwanza kwa hili. Ila... Mungu anamuona.

    ReplyDelete
  4. Jaman hakuna mtu aendae kucheza mpira akiwa na lengo la kumuumiza mwenzie. Hyo ni bahati mbaya tuu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic