July 9, 2020



DARUESH Saliboko, nyota wa Lipuli amesema kuwa wapo tayari kwa mechi ambazo zimebaki kusaka pointi tatu muhimu.

Leo, Lipuli inamenyana na Alliance FC, Uwanja wa Nyamagana ikiwa nafasi ya 16 na pointi 37 huku Alliance ikiwa nafasi ya 17 ikiwa na pointi 37 wakiwa tofauti kwenye idadi ya mabao ya kufunga ambapo Lipuli imefunga mabao 39 na Alliance 27.

Zote zimecheza mechi 33 zinapambani nafasi ya kubaki kwenye ligi msimu ujao kwa kuwa hazipo sehemu salama kwa sasa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Saliboko mwenye mabao 10 ndani ya ligi akiwa ni namba mbili kwa utupiaji ndani ya Lipuli na kinara wao akiwa ni Paul Nonga mwenye mabao 11.

“Tuna kazi kubwa ya kupambana ili kupata matokeo mazuri kwani nafasi ambayo tupo sio salama ni lazima tupambane ili kushinda mechi zetu zilizobaki tunahitaji kubaki kwenye ligi,” alisema.

Timu nne zinashuka jumla msimu huu ambapo tayari moja Singida United imeshakamilisha safari yake ndani ya Ligi Kuu Bara kwa sasa inakamilisha ratiba.

Ipo nafasi ya 20 ikiwa imecheza jumla ya mechi 34 kibindoni ina pointi 15.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic