ZLATAN Ibrahimovic, nyota anayekipiga ndani ya Klabu ya AC Milan amejipa vyeo vikubwa vitatu kwa wakati mmoja kwa kusema yeye ni rais, mchezaji na kocha.
Ibrahimovic ameyasema hayo baada ya kikosi chake kuitungua mabao 4-2 Juventus kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Italia wa 'Serie A' ambapo yeye alitupia bao moja kwenye ushindi huo.
Nyota huyo mwenye miaka 30 amekuwa ni mtu mwenye kauli za kibabe siku zote pale timu yake inapofungwa hata inaposhinda kwani kuna wakati aliwahi kusema kuwa wachezaji walicheza chini cha kiwango baada ya timu yake kufungwa.
Ameongeza kuwa iwapo angewahi kutua ndani ya kikosi hicho ana imani kuwa timu yake ingetwaa ubingwa wa ligi hiyo kwani alitua hapo akitokea Klabu ya LA Galaxy ya Marekani.
"Mimi ni rais, mchezaji na kocha kama ningeanza hapa tangu mwanzo wa msimu tungetwaa ubingwa wa ligi mapema kabisa," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment