July 16, 2020


MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa ushindi walioupata wa mabao 2-1 mbele ya Liverpool ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu England umetokana na juhudi za wachezaji wake uwanjani.

Arteta amesema kuwa haikuwa kazi rahisi kupata ushindi mbele ya mabingwa kwani wana timu imara ya ushindani ambayo imewapa ubingwa.

"Vijana walikuwa na juhudi kazini jambo lililowapa nguvu ya kupata matokeo mazuri mbele ya wapinzani wetu kazi ilikuwa kubwa.

"Kucheza na mabingwa na kupata matokeo ni jambo jema hii inatupa picha ya kujua kule ambako tunakwenda kama si kwa wakati huu basi itakuwa kwa ajili ya wakati ujao," amesema.

Mabao ya Arsenal yalipachikwa kimiani na Alexandre Lacazette dakika ya 32 na Reiss Nelson dakika ya 44 huku lile la kwanza kabisa kuandikwa kwenye mchezo huo lilifungwa na Sadio Mane dakika ya 20.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic