KOCHA Mkuu wa Mbao FC ya Mwanza, Felix Minziro amesema kuwa kinachoibeba timu yake kupata ushindi ni morali kubwa ya wachezaji kwenye kupambana kutafuta matokeo.
Miziro amekiongoza kikosi chake kwenye mechi tatu ambapo ameshinda zote mfululizo jambo ambalo linaifanya Mbao kufufua matumaini ya kubaki kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mchezo wake uliopita, Julai 4 aliinyosha Lipuli ya Iringa mabao 2-0 yaliyopachikwa kimiani yote na Wazir Jr.
Minziro amesema :"Bado kuna ushindani mkubwa ila ninaona vijana wangu wanapambana kwa hali na mali kwenye kusaka matokeo na morali ipo juu nina amini tutashinda mechi zilizobaki na kusalia ndani ya Ligi Kuu Bara."
Mbao FC ipo nafasi ya 19 ikiwa imecheza mechi 33 kibindoni ina pointi 32.
0 COMMENTS:
Post a Comment