July 28, 2020


LICHA ya kubakisha miezi miwili kabla ya mkataba wake kumalizika, kiungo nyota wa Yanga, Haruna Niyonzima, amefunguka kwamba ameamua kuuweka kando mkataba wake mpya na timu hiyo.

Niyonzima amesema ameamua kufanya hivyo kwa kuwa alitaka kwanza wamalize masuala ya ligi kisha aanze mazungumzo na mabosi wake huku akiweka wazi kuwa kama ikishindikana anaweza kuondoka.

Kiungo huyo Mnyarwanda alitua Yanga kipindi cha dirisha dogo Desemba, mwaka jana akitokea AS Kigali ya kwao na kuanguka saini ya miezi sita.

Mnyarwanda huyo amesema kuwa licha ya mkataba wake kwenda kumalizika, lakini kwa sasa ameliweka kando suala.


“Mimi kama mchezaji mkataba wangu unaenda kumalizika hivi karibuni imebaki kama miezi miwili tu lakini siwezi kuzungumzia kwa sasa.

 "Ukiwa mchezaji huwezi kuchagua kambi ila kwa sasa bado siwezi kuzungumzia masuala ya usajili wangu na mkataba wangu ndani ya Yanga," amesema.

2 COMMENTS:

  1. Huna lolote ww kwasshv kwenye timu kubwa

    ReplyDelete
  2. Jitathmini kwa sababu unawakumbuka Yanga vizuri. Ukiwazingua wamechoma moto jezi yenye namba yako bro

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic