MWENDO unazidi kuwa mkali kwa timu ambazo zinapambana kushuka Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na zile ambazo zimeshapata tiketi ya kupanda ndani ya Ligi Kuu Bara.
Tumeshuhudia kwamba vita ya ubingwa imemalizika na Simba kutwaa taji lao ambalo tayari walikabidhiwa rasmi kule Lindi ambapo walicheza na Namungo FC, Julai 8.
Kwa sasa vita inayoendelea ni kwa timu ambazo zinasaka nafasi ya kulinda heshima ili kubaki ndani ya ligi pamoja na nyingine zinahitaji kuwa ndani ya tano bora.
Kwa upande wa Ligi Daraja la Kwanza ile vita ya kumsaka nani atakayepanda daraja imeshaisha ambapo tayari kila kundi lishampata mbabe wao.
Kwenye kundi B ninakukumbusha kwamba Gwambina wao walikuwa wa kwanza kumaliza hesabu za kupanda Ligi Kuu Bara muziki ulikuwa unaendelea kuchezwa kundi A.
Kwenye kundi A kulikuwa na ushindani mkubwa ambapo kila timu ilikuwa inapambana kusaka matokeo chanya hilo ni jema kwani kule kundi B mambo hayo yalikuwepo ila mwisho mambo yakawa magumu kwa Geita ambao wana uhakika wa kucheza play off baada ya kushindwa kupanda kwenye ligi moja kwa moja.
Kundi A ambalo kinara ni Dodoma FC yeye alikuwa anapambana na Ihefu ambaye yupo nafasi ya pili wote wakiwa na pointi 51 baada ya kucheza mechi 22.
Mwisho wa siku Dodoma FC amepenya baada ya kushinda mchezo wake wa mwisho na kumzidi Ihefu kwa idadi ya mabao ya kufunga kwani pointi wote wapo sawa.
Baada ya kupanda sasa ni wakati wa kusoma ramani mambo yatakuwa namna gani huko juu kwani nako kuna ushindani mkubwa kikubwa kujipanga.
Kwa sasa kwenye Ligi Kuu Bara ni lala salama huku kwenye Ligi Daraja la Kwanza timu zinajiandaa kucheza playoff
Katika hili ipo wazi kwamba ni jambo la msingi kupata mshindi ambaye hatapata tabu akipanda ligi msimu ujao wa 2020/21 itasaidia kueleta ushindani mkubwa .
Kwa kuwa hizi ni mechi za mwisho na zina umuhimu mkubwa kwa kila timu kupata matokeo mazuri ambayo yatawafanya wafikie malengo waliyojiwekea.
Kikubwa kinachotakiwa kwa sasa ni kuona kwamba kila timu inafanya maandalizi mazuri ili kupata matokeo mazuri ndani ya uwanja ambayo yatawapa kile ambacho wanakihitaji baada ya dakika 90.
Wapo ambao wamekuwa wanapenda kuleta ugomvi ndani ya uwanja hayo yamepitwa na wakati ni muhimu kutulia na kufanya maamuzi kwa akili zaidi.
Hivyo wale wote ambao watakuwa uwanjani wapambane kutafuta matokeo ndani ya uwanja kupata matokeo chanya.
Kwenye Ligi Daraja la Kwanza tunataka kuona kwamba kila mechi inakuwa na mvuto pamoja na ushindani ule ambao unaonekana kwa kila mmoja kucheza na kupata ushindi.
Tunataka kuona kila timu inapata matokeo ambayo yanastahili kwao na wakimaliza kucheza wafurahiee kile wanachokivuna na baada ya kushuka ama kupanda wasiwe na malalamiko.
Mechi za lala salama ni muhimu maandalizi yakawa mazuri katika kumalizia mechi hizi ambazo zimeshikilia maamuzi ya mechi za mwisho.
Tukija Ligi Kuu Bara ni muhimu kwa kila timu ikawa na uhakika wa kushinda mechi zote za nyumbani na ugenini bila mashaka yoyote.
Ipo nafasi ya kupata matokeo na kujinusuru kwa timu ambazo zina mechi mkononi ikiwa zitachanga vema karata zao kwa mechi abazo zimebaki.
Ikiwa kila mmoja ataamua kufanya vizuri na akapata matokeo mazuri basi zitatimiza ndoto za kubaki kwenye ligi kwa ajili ya msimu ujao na ikishindikana basi zijipange kwa ajili ya maisha ya Ligi Daraja Ligi Daraja la Kwanza.
Kwa zile ambazo zitapanda mpaka kufika ndani ya Ligi Kuu Bara ni lazima zijipange vizuri katika mechi zote ambazo watakutana nazi kwenye maisha mapya wakati ujao.
Tunataka kuona timu zenye ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara na zile ambazo zitashuka daraja zikapambane pia ili kurudi huku ndani ya ligi.
Wasijisahau kwamba wanakwenda kwenye makazi mapya na wengine wanapanda kwenye makazi mapya ni lazima kujipanga vizuri hakuna namna.
Wachezaji wapambane ndani ya uwanja kwa hali na mali kwa ajili ya timu zao ambazo zinahitaji matokeo mazuri muda wote.
Itakuwa vizuri ikiwa kila mmoja atakuwa kwenye kutimiza majukumu yake na apambane kwelikweli kwani ndio kazi yake aifanye kwa ukamilifu bila ulegevu.
Marefa wafuate sheria 17 za mpira katika kusimamia maamuzi yao ili wasiboronge mambo kwani kwenye mechi za lala salama mechi moja ina umuhimu katika kuishusha timu ama kuongeza nguvu.
Yale makelele ambayo yamekuwa yakiskika kwenye mechi ambazo zinachezwa ndani ya uwanja inapaswa ziwekwe kando na kila mmoja akawa anatenda haki.
IIkiwa kila mmoja atatimiza wajibu wake kwa wakati itakuwa rahisi kuwa na timu imara ambazo zitaleta ushindani ndani ya ligi.
0 COMMENTS:
Post a Comment