July 15, 2020


INAELEZWA kuwa wachezaji na benchi la ufundi la Simba leo wamepewa mkwanja wao wa milioni 380 ambao waliahidiwa kupewa kabla ya mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali dhidi ya Yanga.

Simba iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 mbele ya Yanga mchezo uliochezwa Julai 12, Uwanja wa Taifa, Dar.

Kabla ya mchezo awali ilielezwa kuwa kungekuwa na mgawanyiko kwa upande wa mkwanja huo kwa wachezaji wa kikosi cha kwanza na wale ambao wangekaa benchi pamoja na wengine ambao hawakucheza kabisa.

Jambo hilo lilipokelewa tofauti na wachezaji waliocheza mchezo huo na kuomba uongozi uwape wote fedha zinazolingana kwa kuwa ni timu moja.

Hivyo leo wachezaji wote wamevuta mkwanja wa milioni 10 kila mmoja ikiwa ni bonasi ya kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho. 

Simba itakutana na Namungo FC Kwenye mchezo wa fainali unaotarajiwa kuchezwa Agosti 2, Uwanja wa Nelson Mandela. 

Katibu Mkuu wa Simba, Dr. Arnold Kashembe amesema kuwa suala la zawadi kwa wachezaji lipo ila litawekwa wazi wakati ukifika.

5 COMMENTS:

  1. Big up sana wachezaji wa Simba mliocheza mchezo huo, mnajitambua kweli. Ni ukweli kabisa kuwa kila mchezaji ana mchango kwenye ushindi wo wote wa timu, kama hajacheza leo basi alicheza juzi na jana. Hongera La Kapteni Bocco na msaidizi wako Tshabalala

    ReplyDelete
  2. Mikwanja kama hio ya Marakwamara Bila ya kucheleweshwa au wachezaji kuwahi kuhimiza au kukumbusha ndicho kinachowatuliza na kuwajaalia wachezaji kuheshimu, kutulia, kujituma, kuwa na
    morali ya hali ya juu na hata wale waliokuwa hawaupati nafasi za Mara kwa mara, hebu nambie wangapi tangu Moo kukabidhiwa timu wameondoka kwenda kwa Yanga na wangapi wameondoka Yanga kujiunga na SIMBA. Ndio mana wakasema kuminona. Kuna nidhamu na kuheshimiana, Hakuna mchezaji anaezomewa hata akikosea mara kumi na ndio maana wachezaji kama Hao haraka hurejea Katika viwango vyao. Hatujawahi kusikia mchezaji kwenda kushiriki au kugoma kwa kutolipwa haki zake

    ReplyDelete
  3. Unaona ubaguzi huo. Inapocheza Simba humu tunaona full covering lakini leo kwakuwa Yanga wala habari hamna kama vile hamna kitu.

    ReplyDelete
  4. Kuna yeyote bado atamshawishi rashidi juma aondoke aende lipuli ambapo atapata namba ya kudumu au hata na unahodha

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ninamshauri atolewe kwa mkopo kwenye timu iliyo nafasi nzuri lakini pia atakakopata nafasi ya kucheza. Rashid Juma ana kipaji sana na umri haujamtupa mkono sana. Pesa atapata zaidi ya hizo atakapoaminika tena Simba na kuingia kikosi cha kwanza. Akajifue na kunoa kipaji chake kisha arudi nyumbani alikolelea tangu akiwa Simba B

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic