LEO Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea ambapo timu nne zitakuwa kazini kusaka pointi tatu muhimu kwenye viwanja viwili tofauti.
Alliance FC iliyo nafasi ya 17 itaikaribisha Lipuli FC Uwanja wa Nyamagana ambayo ipo nafasi ya 16 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara zote zikiwa zimejikusanyia pointi 37 kibindoni.
Tanzania Prisons iliyo nafasi ya 10 na pointi zake 44 itaikaribisha Coastal Union Uwanja wa Sokoine iliyo nafasi ya tano ikiwa na pointi 48 kibindoni.
Zote zimecheza mechi 33 ndani ya ligi dakika tisini zitaamua nani atasepa na pointi tatu ama kuyeyusha na ikiwa watatoshana nguvu basi wote wataondoka na pointi mojamoja.
0 COMMENTS:
Post a Comment