July 22, 2020



UONGOZI wa Mbao FC umesema kuwa upo tayari kwa mchezo wa leo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC.

Mbao inapambana kubaki ndani ya ligi ikiwa imecheza mechi 36 kibindoni ina pointi 39 hatma yake ya kubaki inategemea matokeo ya wapinzani wake wengine ambao wapo juu yake.

Ndanda iliyo nafasi ya 18 ikiwa na pointi 40 ipo juu yake hivyo ikifuatiwa na Alliance iliyo nafasi ya 17, Mwadui nafasi ya 15 na Mtibwa Sugar iliyo nafasi ya 14 ndizo zimeshikilia hatma ya Mbao ikiwa itashinda leo.

Mwadui FC itamenyana na Biashara United,Mtibwa Sugar itamenyana na Yanga jambo ambalo linaongeza ushindani kwa timu zote ndani ya ligi.

Felix Miziro, Kocha Mkuu wa Mbao FC amesema kuwa watapambana ili kupata matokeo mazuri kuhusu kubaki ama kushuka itajulikana baadaye.

"Tupo kwenye nafasi mbaya ila tunataka kupata ushindi kisha mengine yatafuata, ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji ushindi," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic