July 18, 2020


IMEELEZWA kuwa Klabu ya Grupo Desportivo de Chaves inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Ureno imemtengea winga wa Simba, Luis Miquissone kiasi cha shillingi bilioni 1 ambacho wanaamini kinatosha kuwashawishi Simba kumuachia winga huyo raia wa Msumbiji.

Miquissone tangia atue Simba akitoka katika timu ya UD Songo amekuwa mchezaji muhimu ndani ya kikosi cha Simba jambo ambalo litakuwa gumu kwa Simba kumuachia kutokana na kwenda kushiriki michuano ya kimataifa ya Ligi ya mabingwa Afrika kwa msimu ujao.

Moja kati ya kiongozi mkubwa ndani ya Simba amesema kuwa kuna taarifa ambazo wamezipata kutoka katika timu hiyo ya Ureno ikimuhitaji winga huyo ili kumsajili huku akisema kuwa timu hiyo bado haijatuma ofa hiyo na kwa upande wa Simba bado hawajapokea ofa hiyo.

“Taarifa za Miquissone kuhitajika na Chaves ya Ureno tumezisikia na ni kwa muda mrefu kidogo wamekuwa wakimfuatilia mchezaji huyu na sisi taarifa hizo zimetufikia lakini hadi sasa bado hakuna ofa yeyote iliyotumwa kutoka kwao Ureno kwenda kwa uongozi wa Simba,hivyo bado zinabakia kuwa tetesi kama ambavyo viongozi wanasikia.

“Lakini bado itakuwa ni ngumu kwa Miquissone kuachiwa kirahisi kwa kuwa Simba bado inampango nae ikiwa ni pamoja katika kuhakikisha inafanya vizuri katika mashindano ya kimataifa kwa kuwa kama utakumbuka msimu uliopita Simba haikufanya vizuri,” kilisema chanzo hiko.


Miquissone ametupia jumla ya mabao manne ndani ya Simba akiwa nayo matatu kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na bao moja kwenye Kombe la Shirikisho.

Ana pasi moja ya bao aliyoitoa ndani ya ligi kwa Meddie Kagere wakati Simba ikishinda mabao 3-1 Uwanja wa Taifa.

3 COMMENTS:

  1. wakileta pesa aende maana hyo besa inatosha kupata wachezaji 3 wa kiwango chake

    ReplyDelete
  2. Mpira ni biashara, kama hela ni ndefu auzwe

    ReplyDelete
  3. Kuna tetesi basi sijui ni kweli au kichekesho tu, eti Gongowazi nao pia wanamuhitaji

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic