July 18, 2020


ALLIANCE FC iliyo nafasi ya 14 kwenye msimamo ikiwa na pointi 21 baada ya kucheza mechi 35 haijawahi kusepa na pointi tatu mbele ya Simba.

Imepanda daraja msimu wa 2018/19 kwenye mechi yao ya kwanza kukutana walionja joto ya jiwe kwa kunyooshwa mabao 5-1.

Mchezo wa pili ikapoteza kwa kufungwa mabao 2-0. Msimu wa 2019/20 mchezo wa kwanza, Uwanja wa Kirumba, Simba ilishinda mabao 4-1.

Jumla Simba imeifunga Alliance mabao 11 na imefungwa mabao mawili ndani ya mechi tatu na kesho wanakutana Uwanja wa Taifa. Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili.

Simba haina cha kupoteza baada ya kutwaa taji la ligi ikiwa na pointi 81 kibindoni huku Alliance ikisaka pointi tatu kujinasua kushuka daraja.

Kwenye mchezo huo, Simba watatoa fursa ya mashabiki kupiga picha na taji la ligi ambalo wamelitwaa kwa msimu huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic