July 27, 2020

MANCHESTER United iliyo chini ya Kocha Mkuu, Ole Gunner Solskjaer imehitimisha msimu wa 2019/20 ikiwa ndani ya top 4 ikiwa na uhakika wa kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Bruno Fernandes alianza kupachika bao la kuongoza dakika ya 71 kwa penalti kisha Jesse Lingard bao la pili dakika ya 90+6 wakati wakishinda mabao 2-0 mbele ya Leicester City. 

Leicester City walimaliza wakiwa pungufu baada ya Jonny Evans kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 90+4.

Ushindi huo unaifanya Manchester United kumaliza ikiwa nafasi ya tatu ikiwa na pointi 66 huku Leicester City ikiwa nafasi ya tano na pointi 62.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic