KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameweka wazi kwamba muda wa kuiwaza mechi hiyo bado haujafika kwa kuwa ana mechi ya kucheza kabla ya kuvaana na wapinzani wake hao kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali, Uwanja wa Taifa.
Kocha huyo amefunguka kwamba, amewaweka ‘kiporo’ Yanga kutokana na akili yake kwa sasa kuwaza ya Ligi Kuu Bara iliyo mbele yake kwani anataka kushinda licha ya kwamba tayari wamekuwa mabingwa.
Sven amesema lengo lake kabla ya mechi hiyo ya Julai 12 itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar ni kushinda mechi dhidi ya Jumatano dhidi ya Namungo.
“Kuhusiana na mechi na Yanga, itakuwa ngumu kwa timu zote mbili, lakini kwangu kwa sasa siyo muhimu. Kuna siku zaidi ya tatu kabla ya mechi hii, hivyo basi siwafikirii sana.
“Kwa sasa kilicho mbele ni kuangalia namna gani tunashinda mechi ya ligi. hatutaki kuona tunakosa pointi kwenye mechi yetu licha ya kwamba tumekuwa mabingwa,” amesema Sven.
Simba kesho, Julai 8 itamenyana na Namungo kwenye mchezo utakaochezwa Uwanja wa Majaliwa.
Mbona sijaona mkwara wowote?
ReplyDelete