KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison leo alitumia dakika 64 ndani ya Uwanja wa Taifa huku akidhibitiwa na mabeki wa safu ya Simba iliyokuwa ikiongozwa na Pascal Wawa kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali.
Baada ya Morriosn kutolewa aligoma kukaa benchi na wachezaji wenzake jambo ambalo lilizua taharuki licha ya kurudishwa na mwamuzi wa nje hakutaka kufanya hivyo zaidi ya kuongeza mwendo kuelekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Nafasi ya Morriosn ilichukuliwa na Patrick Sibomana ambaye aliongeza kasi ya mashabulizi kwa Simba na kubadilisha upepo kwa kiasi chake baada ya kuingia uwanjani.
Yanga ilitinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Kagera Sugar mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.
Kufungwa leo mbele ya Simba kumeyeyusha matarajia ya timu hiyo kushiriki michuano ya kimataifa hivyo wana kazi ya kujipanga msimu ujao.
Mchezo wa leo Simba imeshinda mabao 4-1 na unawapa tiketi ya kusonga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho ambapo watacheza na Namungo FC ya Lindi.
Fainali inatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga ambapo bingwa wa msimu uliopita alipatikana Uwanja wa Ilulu ambaye ni Azam FC.
Azam FC ilitolewa na Simba hatua ya nusu fainali kwa kufungwa mabao 2-0 mchezo ulichezwa Uwanja wa Taifa.
Ameanza kuwa panda tena morisoni ata watowa damu utopolo fc, simba ni kisanga Moto mkali sana 🔥🔥🔥🔥
ReplyDeleteMuandishi anawasifu Gongowazi eti baada ya Kutoka Morrison na kuingia Patrick Sibona Yanga ilianza kuliandama lango la Simba. Mimi najiuliza wakati gani waliliandama lango la Simba? HAHAHAAA
ReplyDeleteKama ada yao Yanga walianza kumzomea Morrison na kumrushia chupa na kabla ya hapo wakimshangilia na wengine wakimsifu kwa kitumbuwa Simba kwa bao la Tarihi
ReplyDeleteTulisema sana kitendo cha kumsifia kupita kiasi kilimfanya awaone yanga wanamwabudu akavimba bichwa. Sasa kazi kwenu, huyu hana nia ya kuendelea yanga matarajio yake hasa ya kifedha hayajatimia. Pia kwa vile yanga haichezi international next year ndio kabisaaa hakai huyo
ReplyDeleteMbona wamesahau kichwa cha habari Morison muuaji wa Simba
ReplyDelete4G Full majanga Yanga Jangwani
ReplyDeleteGSM wanajaribu kujaza maji ndani ya kumuto
ReplyDelete